Monday, December 9, 2013

IBADA YA SIFA, KUABUDU NA MAOMBI

VIONGOZI WA IBADA

WAUMINI WAKIWA IBADANI

MTUMISHI SHADRACK AKIHUDUMU

MUIMBAJI BINAFSI AKIHUDUMU

WAHUDUMU WA MITAMBO


Monday, December 2, 2013

MESSAGE FROM BISHOP D. KAGANGA


BISHOP DICKSON KAGANGA , HIS WIFE AND CHURCH MEMBERS 

My theme was the problem faces the body of Christ today in which some ministers are almost demanding to be worshiped....
The Bible portray the church as the "bride" whereby Jesus is the "groom"
Now, in Jewish culture this was well known ideology. When a Jewish young man was engaged to a woman... It was custom for them to leave and go far to work and earn money as preparation to get married. When a bride goes - he trust one of his close friend to take care her. One of the duties of a friend was to encourage the bride.... "Don't worry, I know my friend, he is faithful and hard working person... He will definitely return..."
Problems:1. Some friends were unfaithful and TRAITORS. Instead of speaking for the bride they spoke for themselves... "Look how much I care, It is me who is doing this and that for you..."
2. Some brides forgot to think of the groom and started to give focus to a friend....
My fellow leaders.... Jesus says that he has gone but he will come again (John 14:2, 3). Therefore, let's glorify God. Let's tell our people that we are just friends of Jesus... We are not the grooms....
Members, we may do a lot in your life, but let's our focus be in Jesus (Heb. 12:3)

Sunday, December 1, 2013

MAMIA WAHUDHURIA IBADA YA SIKU YA WABABA CCC ZANZIBAR

WASHARIKA IBADANI

WASHARIKA WAKIWA IBADANI

WABABA WAKIWA WAKATI WA SIFA

WABABA WAKIIMBA

WABABA WAKIIMBA

WABABA WAKIIMBA

WAKATI WA MAOMBI

Thursday, November 28, 2013

HARUSI MBILI ZAFUNGWA TAREHE 24/11/2013 CCC KARIAKOO ZANZIBAR

MAHARUSI WAKIWA KANISANI

MCHUNGAJI KHALFAN AKIWA TAYARI KWA IBADA 


MOJA YA WANANDOA WAKILA KIAPO

WAKATI WA MAHUBIRI

IBADA YA SIFA 24/10/2013 CCC KARIAKOO ZANZIBAR

WAGENI WALIOHUDHURIA IBADA YA JUMAPILI
WAHUDUMU WA IBADA KWAYA YA ZAC
MCHUNGAJI MARY AKIONGEA NA WAGENI WETU
WAKATI WA MAOMBEZI 
ZAC WAKIHUDUMU

Tuesday, November 26, 2013

BISHOP DICKSON KAGANGA OUT OF ZANZIBAR SERVICES


BISHOP DICKSON (LEFT) DURING THE SERVICES OUT OF ZANZIBAR.HE IS THE DIRECTOR FOR THE MISSIONARY DIRECTORATE IN TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD.


BISHOP D. KAGANGA (RIGHT) WITH HIS FELLOW PASTORS ATTENDING MEETING

BISHOP DR MTOKAMBALI (THE HEAD OF TAG) ADDRESSING ISSUES DURING THE MEETING WHERE BISHOP D KAGANGA (LEFT) IS THE MEMBER OF THE CENTRAL COUNCIL OF TAG

BISHOP D. KAGANGA DURING THE MISSIONARY ACTIVITIES

JE,MKRISTO (ALIYEOKOKA) NI VYEMA KUOA AU KUOLEWA NA MTU ASIYEOKOKA (ASIYE MKRISTO)?

Utangulizi:Katika kujibu swali hili, itabidi kwanza tujifunze mambo yanayojitokeza katika swali:
1) Mkristo ni nani2) Asiye Mkristo ni nani3) Ndoa ya Kikristo ikoje.
1) Mkristo ni: a: Mtu aliyekubali kumpokea Yesu Kristo na kuamini kuwa ni Bwana na mwokozi wa maisha yake; na mtu huyu ndiye anayepewa uwezo wa kufanyika mtoto wa Mungu (Yn.1:12).
b: Mfuasi/Mwanafunzi/Mtu wa Kristo ( ndivyo wenyeji wa Antiokia walivyowaita-Mdo.11:26) au ni mtu aliyezaliwa mara ya pili (aliyeokoka).
c: Kiungo (Efe.4:25) katika mwili wa Kristo (sehemu ya Kanisa).
d: Hekalu la Mungu ambalo Roho Mtakatifu anakaa ndani yake (1Kor.3:16; 6:16; 2Kor.6:16). 
2) Asiye Mkristo ni kinyume cha Mkristo, yaani:a: Mtu anayekataa kumpokea Yesu Kristo na kutoamini kuwa Yesu ndiye Bwana na mwokozi wa maisha yake; na mtu huyu ndiye anayetembea katika hukumu ya adhabu (Mk.16:16; Rum.8:1).
b: Mtu ambaye si mfuasi wa Kristo au ambaye hajazaliwa mara ya pili.
c: Mtu ambaye si kiungo katika mwili wa Kristo ( si sehemu ya Kanisa).
d: Mtu ambaye si hekalu la Mungu, hivyo Roho Mtakatifu hawezi kukaa ndani yake.
3) Ndoa ya Kikristo ni:Agano (siyo mkataba) kati ya mume na mke (wa-Kristo) kuishi pamoja maisha yao yote bila kuachana (Mk.10:8,9; Mal. 2:16).
Sasa hebu tujifunze zaidi juu ya jambo hili kwa kutafakari maandiko yafuatayo:a: Zab.133:1; inasomeka “ Tazama,jinsi ilivyo vema, na kupendeza, Ndugu (walioamini/wanandoa) wakae PAMOJA, kwa UMOJA”. Maana yake hapa, nikwamba walioamini/wanandoa wanatakiwa kukaa PAMOJA kimwili (kufanya mambo kwa pamoja) na kwa UMOJA wa Roho (Efe.4:3; Mw.2:18). Umoja wa Roho ndio unaotufanya tuwe katika Mwili (Kanisa) mmoja, Roho mmoja, Tumaini moja, Bwana (Yesu) mmoja, Imani (Ukristo) moja, Ubatizo (wa maji mengi) mmoja na Mungu (Yehova) mmoja (Efe.4:4-6).
Ukurasa 1b: Mw.24:3,4 . Ukisoma maandiko haya utaona kuwa Mzee Ibrahimu alipotaka kumwozesha mtoto wake Isaka alikataa kumtwalia mke katika binti za Wakanaani aliokuwa anakaa kati yao, badala yake alitaka atwaliwe mke kutoka katika nchi yake na kwa jamaa zake.
Ebu tukajiulize swali kidogo hapa; hivi, ni kwanini Ibrahimu aliongozwa na Mungu kumchukulia mke mtoto wake kutoka katika nchi yake na kwa jamaa zake badala ya nchi ya Kanaani?Jibu:i: Kwakuwa Ibrahimu alikuwa ni Mwebrania (Mw.14:13), alitaka mtoto wake apate mke kutoka kwa waebrania badala ya kuchukua mke kutoka kwenye makabila mengine. (Kwa sasa tungesema “Kwakuwa mtu amekuwa Mkristo, anatakiwa mtoto wake apate mke/mume kutoka kwa Wakristo badala ya kuchukua mke/mume kutoka kwenye imani zingine”).ii: Kwakuwa Mungu alikuwa amefanya AGANO la milele na Ibrahimu (agano jipya na wanaoamini kwa sasa) na uzao wake (Mw.17:1-8), na wala hakufanya Agano na mataifa mengine (wasioamini kwa sasa), na kwa kuwa mataifa hayo yalikuwa yanaabudu miungu/masanamu; hivyo mzee Ibrahimu aliona kumchukua mke nje ya Agano kwaajili ya mtoto (Isaka) wake ni kuchafua Agano lake na Mungu.iii: Kwakuwa Wakanaani walikuwa watu wa mataifa wasiomjua Mungu (wasiookoka kwa sasa), walikuwa chini ya laana (hukumu kwa sasa=Mk 16:16); na kwasababu hiyo mzee Ibrahimu aliona kumchukua mke kutoka kwa watu walio chini ya laana ni kukaribisha LAANA katika jamii ya WAEBRANIA (wa-Kristo kwa sasa).c: Kut.34:12-16. Ukisoma maandiko haya utaona kuwa Mungu anamuasa Musa kwamba asifanye Agano na wenyeji wanchi ya Kanaani ili watu wa Mungu (wana wa Izraeli) wasije wakafanya UZINZI na miungu yao, pia WASIWAOZE WANA (wavulana) WAO BINTI ZAO, NAO BINTI ZAO ili wasije wakashiriki kufanya UZINZI na miungu yao. d: 2Kor.6:14-16. Ukisoma maandiko haya utaona mtume Paulo akiongozwa na Roho anawaasa waumini (Kanisa) wa Korintho kwakusema “ (mlioamini/mliookoka) Msifungiwe nira (msioane) pamoja na wasioamini (wasiookoka), kwajinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya HAKI (wokovu) na UASI (dhambi)? Tena pana shirika gani kati ya NURU (Mkrito) na GIZA (asiye Mkristo)? Tena pana ulinganifu gani kati ya KRISTO na BELIARI (shetani)? Au yeye AAMINIYE (aliyeokoka) ana sehemu gani pamoja na yeye ASIYEAMINI? Tena pana mapatano gani kati ya HEKALU (Mkristo) la Mungu na SANAMU? Kwa maana sisi (Kanisa) tu hekalu la Mungu aliye hai; …” HITIMISHOMtu wa Mungu; nakusihi katika jina la Yesu; usije kuingia kwenye jaribu la kumtafuta mwenzi wako wa maisha nje ya Waebrania, Agano lako na Mungu katika Yesu Kristo, Mwili wa Kristo (Kanisani); vinginevyo utajuta na utajikuta unaingia kwenye jaribu jingine la kutafuta ufunguo wako mwenyewe wa kuacha/kutoa talaka ambavyo hairuhusiwi ki-Biblia (Mal 2:16;Mt 19:6;Mk 10:9); au utajikuta unaubeba msalaba wako katika maisha yako yote ya ndoa; na ukifanya mchezo unaweza kujikuta unauacha wokovu.Ukurasa 2Tambua ya kwamba ili kumpata mwenzi wako wa maisha huitaji kwenda kwa msisimko au tamaa ya mwili bali unahitaji kutulia mbele za Mungu ili upate uongozi wa Roho Mtakatifu katika kumpata aliye wakufanana nawe (mwili mmoja, Roho mmoja, Tumaini moja, Bwana mmoja, Imani moja, Ubatizo mmoja na Mungu mmoja -Efe.4:4-6); basi wote mkiwa na mambo hayo saba ktk ndoa yenu, huko ndiko kufanana Mungu alikokukusudia na wala siyo kufanana kwa jinsi ya mwili wa nyama, kwa jinsi hiyo hatimaye wote mtanyakuliwa pamoja na kuishi ktk uzima wa milele kwa pamoja.Ninachoweza kukuhakishia na kukutia moyo ni kwamba, utambue ya kwamba KILA MTU ANAYE WAKWAKE WA KUFANANA NAYE; kama Adamu alikaa miaka mingi katika bustani ya edeni bila kudhihirishiwa mke wake Eva, na hatimaye akadhihirishiwa, basi na wewe usiwe na hofu hata kama unaona miaka imepita. Na ikitokea hukupata neema ya kumpata wakufanana naye, basi muombe Mungu ili ufanane na Yesu hatimaye uishi naye milele kuanzia duniani duniani na hata mbinguni.Mungu akubariki sanaaaaaaaaaaaaaaaaa.Mwl.Majidu KalokolaMob: 0713227861; 0767227861Email: majidukalokola@yahoo.com